Video ya wimbo mpya wa Vanessa Mdee ‘Never Ever’ kutambulishwa Trace Urban (Oct. 9 )
Wakati tunasubiri single yake mpya (audio) kuachiwa rasmi Jumatatu Ijayo, surprise nyingine kutoka kwa Vanessa Mdee ni kuwa video ya wimbo huo ‘Never Ever’ itatambulishwa exclusive na kituo cha runinga cha Ufaransa – Trace Urban leo Oct.9.
Vanessa ambaye tayari yuko Dallas, Marekani alikoenda kuhudhuria tuzo za Afrimma ameshare taarifa hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
“Landed safe in Dallas, Glory to God. Also … catch the #NeverEver video for the first time on @tracenigeria @trace_urban tomorrow Directed by @gorilla_films @icandicam” Vee Money aliandika Instagram.
Video hiyo iliyofanywa na kampuni ya Gorilla Films ya Afrika Kusini chini ya mwongozaji wake Justin Campos itaoneshwa leo saa 2 na dakika 53 asubuhi (8:53AM) kwa saa za Afrika mashariki.
Post a Comment