Image result for tigo banner

Beyoncé afunga mitaa ya New Orleans kushoot video mpya

Ni miaka miwili sasa tangu Beyoncé atoe albamu ya kushtukiza na dunia nzima kupagawa.
beyonce-jpeg
Lakini huenda Queen B akawa na surprise nyingine kubwa.
Kwasababu malkia huyo alikodi uwanja wa Mercedes-Benz Superdome huko New Orleans kwa kushoot video mpya Jumanne hii. Aliingia kwenye uwanja huo akiwa na mume wake Jay Z.
Haijulikani hasa nini alichoshoot lakini hivi karibuni amekuwa akionekana kwenye mji huo akiwa na mumewe na mwanae Blue Ivy.
Wikiendi iliyopita alifunga mitaa kadhaa ya mji huo kushoot.
“Beyonce is shooting a video in new Orleans and just had the street cameras turned off. The entire area. What a god,” shabiki mmoja alitweet.

No comments

Powered by Blogger.