Messi na Neymar wapigwa chini kikosi bora cha makundi UEFA, Fahamu kikosi kamili
Kikosi bora cha wachezaji kumi na
mmoja kilichocheza hatua ya makundi ya michuano ya Klabu Bingwa Ulaya
kimetangazwa na Uefa jambo la kushangaza likiwa kuachwa nje kwa nyota wa
Barcelona Lionnel Messi, Neymar na Luis Suarez.
Washambuliaji Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Hulk (Zenit St
Petersburg) pamoja na Thomas Muller (Bayern Munich) ndio wanaoongoza
safu ya ushambuliaji, kikosi hicho kikitumia mfumo wa 4-3-3.Ligi Kuu ya Uingereza imetoa wachezaji wawili, sawa na ligi ya Ujerumani na ile ya Ufaransa.
Mabingwa watetezi wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Barcelona, hawajatoa hata mchezaji moja katika kikosi hicho licha ya kuwa na safu kiwembe ya ushambuliaji.
Hiki ndio kikosi Kamili:
Kipa: Kevin Trapp (Paris Saint-Germain
Mabeki: Andrea Barzagli (Juventus),Thiago Silva (Paris Saint-Germain), Diego Godin (Atletico Madrid), David Alaba (Bayern Munich)
Viungo wa Kati: Sven Kums (Gent), Willian (Chelsea), Raheem Sterling (Manchester City)
Washambuliaji: Thomas Muller (Bayern Munich), Hulk (Zenit St Petersburg), Cristiano Ronaldo (Real Madrid).
Post a Comment