Image result for tigo banner

Weusi waeleza sababu za kwanini mwaka huu hawajatoa kazi ya kundi


Kundi la Weusi linaloundwa na Nikki Wa Pili, G-Nako, Joh Makini, Lord Eyez na Bonta limeeleza sababu za kwanini mwaka huu hawajatoa wimbo wowote wa kundi, mbali na single za mmoja mmoja ambazo hata hivyo kila mmoja zimemsaidia kumuweka pazuri zaidi.

Weusi
Baadhi ya nyimbo walizotoa Weusi kama msanii mmoja mmoja mwaka huu ni kama Joh Makini ametoa Nusu Nusuna Don’t Bother, Nikki Wa Pili ametoa Safari na Baba Swalehe, G- Nako ametoa Laini na anatarajia kuachia wimbo mpya Original, Bonta pia anategemea kutoa kazi mpya.
Msemaji wa kundi hilo, Nikki Wa Pili ametoa sababu za kutotoa kazi ya kundi kwa mwaka huu.
“Mwaka huu Weusi hatujafanya kazi ya kundi ukiacha Gere ya mwaka jana,” alisema Nikki. “Sisi msingi wa kampuni yetu ni kutengeneza msanii mmoja mmoja kuliko kundi, mkitengeneza sana brand ya kundi mkasahau individual kundi likija kuanguka wote mnaanguka, halafu sisi hiyo kwetu hatutaki ije itokee, Nikki wa Pili anatakiwa uwepo wake usitegemee uwepo wa Weusi, au Joh Makini uwepo wake usitegemee Weusi au G-Nako, Kwahiyo sisi kwanza individually ni brand moja moja ndo linakuja kundi.”
Nikki aliendelea,
“Kwa mwaka huu plan ya kazi ya kundi ilikuwa ni ndogo sana kulingana na kulikuwa na msongamano wa project ya mtu mmoja mmoja na mazingira pia ya kampeni yalitokea, mwaka huu Weusi imefocus kazi ya mtu mmoja mmoja.”alimaliza Nikki

No comments

Powered by Blogger.