Image result for tigo banner

Usiende Mbali ya Nedy Music na Ommy Dimpoz yavutia views 1M ndani ya wiki 2

Si kitu rahisi kwa msanii anayechipukia kupata views milioni moja ya video yake kwenye mtandao wa Youtube ndani ya wiki mbili.
13259093_181271122268520_1097302307_n
Lakini imetokea kwa msanii wa PKP, Nedy Music ambaye video ya wimbo wake Usiende Mbali aliomshirikisha bosi wake Ommy Dimpoz imefikia mafanikio hayo.
“1 MILLION VIEWS 1000000+… Ndani ya Siku 13,” ameandika Nedy kwenye Instagram kusherehekea matunda hayo.
189a6f14-43ec-419b-b56f-44a5a02dd53b
“Shukrani za dhati ziende kwa mungu mwenyezi tangia nlipotoka mpka sasa nilipo, pili kwa management yangu nzima ya PKP,” ameongeza.
“Tatu sitoacha kushukuru na kusema ya moyoni kwa wadau wote ambao wanasapoti kazi za kijana wenu tangia nimeanza mpaka sasa siku hadi siku, Ahsanteni sana na sitawaangusha. #USIENDEMBALI BY @NEDYMUSIC FT @OMMYDIMPOZ . Mungu awe nanyi nawapenda sana sana.”
Wimbo huo haujaishia kuangalia tu sana kwenye Youtube bali pia unafanya vizuri kwenye TV za nje.
412dcea6-ae97-471a-8ea6-c7e0510e0bf9
893d1ed1-9590-4a84-8b5b-46f5233328a9
Hadi sasa wimbo huo umekamata nafasi ya 9 kwenye chati za Afrika Mashariki za Soundcity. Pia video yake inapata airtime ya kutosha Trace TV.

No comments

Powered by Blogger.