Wolper adai amefilisiwa na Mkongo , amejikuta hana gari wala sehemu ya kulala
Msanii wa filamu, Jacqueline Wolper baada ya kukiri kwamba anatoka
kimapenzi na Harmonize, amefunguka na kueleza madai ya kufilisiwa na
Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake wa zamani.
Akiongea katika promo ya kipindi kipya cha Take One ambacho
kinatarajiwa kuruka Jumanne hii, Wolper amedai yeye ndiye aliyetendwa na
Mkongo ambaye alikuwa mpenzi wake, kwani wakati anaanza naye mahusiano
alikuwa ana gari na nyumba lakini baadae akijikuta hana hata sehemu
yakulala.
Muigizaji huyo ambaye amekuwa akionyesha uwezo mkubwa katika filamu
zake, amedai alikuwa anajilipia nyumba kwa dola, lakini ulifikia wakati
akafilisika na kuanza kulala hoteli.
Wolper amedai mahusiano hayo yalimsababishia kugombana na baadhi ya
watu wake wa karibu ambao walikuwa wakimshauri vizuri, lakini yeye
alikuwa akiwaaona kama wanamfitini.
Muigizaji huyo ambaye amewahi kutamba na filamu yake Tom Boy, kwa
sasa anatoka kimapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’, Harmonize kutoka
WCB
Post a Comment