Messi atangaza kustaafu soka la Kimataifa, haya ni mambo 17 usiyoyafahamu kuhusu yeye.
Tarehe 24 Juni
2016 gwiji wa soka wa timu ta Argentina na Barcelona aliadhimisha siku
yake ya kuzaliwa. Lakini pia baada ya Fainali ya Copa America ya jana
ambapo Argentina walipoteza kwa kufungwa kwa penati 4-2 dhidi ya Chile,
Lionel Messi ametangaza rasmi kustaafu soka la kimataifa.
Messi amesema kuwa aliwaza sana akiwa katika chumba cha kubadilishia nguo na kusema kuwa amefanya vyote anavyoweza lakini inauma sana kutokuwa mshindi. Alisema kuwa ameshiriki fainali ambazo zimemuumiza sana aliposhindwa kuiwezesha Argentina kutwaa ubingwa.
Haya hapa ni mambo 17 ambayo huenda huyafahamu kuhusu Lionel Messi.

2. Akiwa na umri wa miaka 11, alifanyiwa upasuaji baada ya kusumbuliwa na matatizo ya homoni za ukuaji. Homoni hizo zilikuwa zikizuia ukuaji wake na wazazi wake hawakuweza kulipia gharama za upasuaji huo ambao ilikuwa ni USD 900.

3. Akiwa na umri wa miaka 17, aliweka historia kwa kuwa mchezaji mdogo zaidi kuifungia Barcelona goli.

4. Kiongozi wa Barcelona Carles Rexach alifurahishwa sana na ujuzi wa Messi uwanjani, na aliahidi kuihamishia familia yake nchini Hispania na kulipa gharama za matibabu yake wakati Messi akiwa na miaka 13. Aliandika mkataba wake kwenye napkin sababu ya ukosefu wa karatasi.

5. Mchezo wake wa kwanza alikaa uwanja sekunde 47 tu baada ya kupewa kadi nyekundu alipoingia akitokea benchi.

6. Unafahamu kuwa Messi pia ana medali ya michuano ya Olimpiki iliyopigwa 2008 nchini China?

7. Mwaka 2008 Messi alirithi jezi namba 10 kutoka kwa bingwa Ronaldinho kutoka Brazil.

8. Katika miaka 100 iliyopita, Messi ni mchezaji pekee kufunga magoli 25 katika kalenda ya mwaka kwa klabu yake na timu ya taifa.

9. Alishawahi kupewa nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya Hispania lakini alikataa.

10. Kama kwa sababu yeyote ile Barcelona watavunja mkataba wake na Messi, watatakiwa kumlipa zaidi ya USD 330 milioni.

11. Messi ni balozi wa huruma wa UNICEF, lakini pia huwa anawasaidia watu waliougua ugonjwa wa Fragile X Syndrome (a type of autism).

12. Mara zote anapofunga goli huwa anashangilia kwa kunyanyua mikono yake juu na kutingisha vidole kama kumkumbuka bibi yake aliyefariki akiwa na umri wa miaka 10.

13. Mguu wa kushoto wa Messi ulitumiaka kutengenezea kiatua cha dhahabu Japan chanye uzito wa kilogram 25 ambacho kiliingizwa sokoni ili kuwasaidia wahanga wa tetemeko la ardhi na tsunami. Thamani yake ilikuwa ni USD milioni 5.25

14. Yeye ndiye mfungaji bora wa hat-trick katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

15. Ameshinda mataji matano ya Ballon d’Or. Kati ya hizo, nne alishinda mfululizo tangu mwaka 2009 hadi 2012.

16. Akiwa na umri wa miaka 25, alikuwa mchezaji mdogo zaidi kufunga magoli 200 au zaidi katika ligi kuu nchini Hispania.

17. Messi hapendi kuangalia matukio yake mwenyewe uwanja.

- Messi amezaliwa sehemu moja (Risario) na mwanamapinduzi Che Guevara.

Post a Comment