Image result for tigo banner

Mayunga aitetea video ya limbo wake ‘Please Don’t Go Away’, adai lengo lilikuwa kubeba uhalisia

Mshindi wa shindano na Airtel Trace Music Star 2015, Mayunga ameitetea video ya wimbo wake ‘Please Don’t Go Away’ aliyomshirikisha Akon.

Mayunga 25793877_n

Watanzania wengi wameonesha kutoridhika na video hiyo wakidai haiendani na ukubwa wa wimbo wake na kwamba inaonekana kama documentary.

“Ile ilikuwa makusudi kuifanya vile. Tanzania nyinyi mnanifahamu vizuri kuliko nje kwahiyo ninyi ni watu wa kwanza ambao mnatakiwa mfahamu kwamba ‘dah kwamba maskini huyu mtu ameweza kutoka, hatimaye kafanikisha hiki kitu.’ Na kingine labda watu wamekiona hakipo ni kwamba walitegemea kumuona Mayunga akiimba. Ule wimbo kwa jinsi ambavyo ulivyo kiukweli mimi ilibidi nifuate vile ambavyo walitaka,” Mayunga alisema kwenye kipindi cha Chill na Sky.

Amedai kuwa video hiyo walitaka ioneshe uhalisia wa safari yake kimuziki hadi kukutana na Akon na kurekodi naye wimbo. Amedai kuwa kama angetaka video yake iwe na magari ya kifahari isingekuwa kitu kigumu kwakuwa hata Akon mwenyewe ana lundo la magari hayo.

Mayunga ameongeza kuwa kwenye video zijazo Watanzania wataona hicho wanachokitaka. Sikiliza kipindi cha Chill na Sky hapo chini.

No comments

Powered by Blogger.