Image result for tigo banner

PSG na Real Madrid wako kwenye mazungumzo ya kumsajili Jese Japo kuwa ye Anaitaka Liverpool

Jese-rodriguez
PSG na Real Madrid wako kwenye mazungumzo ya kumsajili Jese Japo kuwa ye Anaitaka Liverpool
Mshambuliaji wa Real Madrid Jese Rodriguez anategemea kuhama mabingwa wa ligi ya Ulaya Real Madrid. Jese amekaa benchi kwa michezo mingi iliyo chezwa na mabingwa hao. Japo kuwa alikuwa anasumbuliwa na majeraha ila hakuweza kupata mda mwingi wa kucheza alipo pona.
Jese anamua kutoka Real Madrid ili kipaji chake cha kucheza kisiweze kupotea. Vyombo vya habari mchana wa leo vimeripoti kuwa Klabu ya Ufaransa Paris Saint German (PSG) wako mbioni kunasa saini ya mshambuliaji huyo japo kuwa mchezaji huyo amesema anataka kujiunga na majogoo Liverpool Fc. Jese anahitajika ili aweze kutengeneza safu ya ushambuliaji akiwa na Cavan baada ya kuondoka kwa Ibrahmovic.
Dalili za wazi zinaonyesha kuwa Jese atajiunga na PSG kwa kuwa kocha wa PSG Unai Emery anampenda  mshambuliaji huyo maana alitaka kumsajili kipindi alipo kuwa kocha wa Sevilla.
 

No comments

Powered by Blogger.