Image result for tigo banner

Maneno ya mimi kumzidi umri Iyobo yananiumiza sana kwa kweli – Aunty Ezekiel

Muigizaji wa filamu za Bongo, Aunty Ezekiel amezungumzia jinsi anavyokerwa na kuumizwa na maneno ya watu wanaouandama uhusiano wake na mzazi mwenzake Mose Iyobo.
aunty
Aunty amesema kuwa anashangazwa na watu wanaomsema kuhusu kumzidi umri Iyobo, kitu ambacho kwake hakimsumbui.
“Kwani wakati tunatongozana hatukujua kuwa tunazidiana umri? Mbona watu wanashindwa kufanya mambo ya msingi na kukalia majungu?” aliuliza Aunty alipohojiwa na Global Publishers.
Ameahidi kulinda uhusiano wake na Iyobo ambaye ni miongoni mwa dancers wa Diamond licha ya kuandamwa na maneno.
“Kwetu sisi suala la umri ni namba tu, labda nikuulize, ulishaona mtoto anambebesha mwanamke mimba? Maneno ya mimi kumzidi umri Iyobo yananiumiza sana kwa kweli, lakini nitaulinda uhusiano huu hadi mwisho,” alisema Aunt Ezekiel.
Chanzo: GPL

No comments

Powered by Blogger.