Image result for tigo banner

Mbwana Aly Samatta amekuwa gumzo Afrika.


Mbwana Aly Samata *SamaGoal* amekuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanao cheza ndani Afrika. Samatta alikuwa mfugaji bora klabu bigwa Afrika na baada ya kuchukua ubingwa huo akiwa na klabu ya TP-Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Baba yake akihojiwa na vyombo vya habari anadai alilia kwa mda wa sas zima,pia mama yake Mbwana alipata mshutuko baada ya kupata habari kuwa mwanae amekuwa mchezaji bora Afrika.

 Mbwana Aly Samatta akiwa amelala na tu yake huku amejifunika bendera ya Taifa la Tanzanaia.

Pierre Aubomeyang mchezaji kutoka Gaboni na Dortmond ya Ujerumani amekuwa mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wanao cheza nje ya Afrika. Gaboni hakika wamempa mapokezi ya kutosha hadi raisi wa nchi ameweka picha za mapokezi hayo kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Shaffih Dauda mchambuzi wa soka Tanzania akiwa na mchezaji bora wa Afrika. Juzi kabla ya tuzo hizo.

Tanzania pia TFF waneshindwa kuandaa vizuri na kuhamasisha watanzania twende kumpokea shujaa wetu wa Kitanzania maana ameleta heshima nchini kwetu pia ameitangaza Tanzania nje ya nchi vyema. TFF walishindwa kupata makubaliano na CAF ili Mbana aweze kufika Tanzania ahsubuhi au mchana. Taarifa zilizopo ni kwamba Samatta amefika nchini saa nane usiku. Kwa mujibu wa taarifa iyowekwa jana kwenye TWITTER na Rais wa TFF bwana Jamal Malinzi.


Baadhi ya vyombo vya habari Afrika vilimpa Samatta uraia wa Nchi nyingi sana. Ikiwepo DRC ya Congo. Hii ilidhihirisha kabisa kuwa Tanzania ilikuwa haitarajii kumpata mtu kama huyu.


No comments

Powered by Blogger.