Niligundua Harmonize alikuwa ananipenda lakini alikuwa anashindwa kuniambia – Wolper
Msanii wa filamu Jacqueline Wolper ameweka wazi jinsi yalivyoanza
mahusiano yake ya mapenzi na hit maker wa wimbo ‘Bado’ Harmonize kutoka
WCB.
Akizungumza Jumatano hii katika kipindi cha Take One Cha Clouds TV,
Wolper amesema alitokewa na Harmonize wakati sahihi ambapo ameshaachana
na mkongo wake ambaye alivyalisha pete.
“Rajabu (Harmonize) sijamjua hivi karibuni, nimemjua siku nyingi sana
na nilikuwa namchukulia kama wasanii wengine wa muziki,” alisema
Wopler.
“Lakini kwa mimi nilikuja kugundua Rajabu alikuwa ananikubali siku
nyingi, tukawa marafiki. Lakini katika kumbukumbu zangu na vitu ambavyo
nimevipitia, naamini kwamba Rajabu alikuwa anashindwa kuniambia. Lakini
alikuja kunitamkia mimi wakati nipo kwenye wakati mgumu sana, kwa hiyo
tukajikuta kunakuwa marafiki na baadae wapenzi,” aliongeza.
Wopler amesema ana mwezi mmoja na wiki mbili toka aingie rasmi kwenye mahusiano ya mapenzi na Harmonize.
Post a Comment