Katika uzinduzi wa nembo mpya ya TTCL, Waziri Mbarawa amesema “TTCL lazima mubadilike ili muweze kuendana na kasi ya mabadiliko ya sayansi na teknolojia na hivyo kumudu ushindani uliopo sasa katika sekta ya mawasiliano.”

FO1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), na wadau wa Sekta ya Mawasiliano (hawapo pichani), wakati uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

FO2 
Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bi. Edwina Lupembe akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE

FO3 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura akielezea mafanikio ya TTCL kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani), katika hafla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

FO4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizindua nembo mpya ya Kampuni ya Simu ya Tanzania (TTCL), jijini Dar es Salam.

FO5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akijadiliana jambo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Dkt. Kamugisha Kazaura, wakati wa halfla ya uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.

FO6 
Baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wakifatilia sherehe za uzinduzi wa nembo mpya ya kampuni hiyo na huduma ya 4G LTE jijini Dar es Salaam.