Image result for tigo banner

Samatta kucheza Europa League mwakani

Mbwana Samatta wa tatu kutoka kushoto waliokaa, akiwa na wachezaji wenzake wakishangilia ushindi wa kufuzu Europa league.

Mtanzania Mbwana Ally Samatta anatarajiwa kucheza michuano ya Europa League mwakani, baada ya timu yake KRC Genk kufuzu kufuatia ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Sporting Charleroi Uwanja wa Cristal Arena, Genk.

Kutokana na matokeo hayo, KRC Genk inafuzu Europa League kwa ushindi wa jumla wa 5-3, baada ya Ijumaa kufungwa 2-0 ugenini katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania nafasi ya mwisho ya Europa League nchini Ubelgiji.

Samatta leo alikuwa ana mchango wake katika tiketi ya Europa League kwa KRC Genk, alifunga bao moja na kusababisha penalti huku akicheza kwa kiwango cha juu.

No comments

Powered by Blogger.